Pages

Subscribe:

Friday, January 22, 2016

MSAMI: IRENE UWOYA BADO ANANIPENDA

Irene Uwoya akiwa na mpenzi wake Msami (600x400)


Msanii wa muziki ambaye pia ni mwalimu wa dance, Msami amesema bado anapendana na Irene Uwoya.
Msami aliiambia Ayo TV Junatano hii kuwa kila siku amekuwa akiambiwa anapendwa na mwanadada huyo. “Najua kwamba ananipenda na amekuwa akiniambia mara nyingi mpaka...
kesho ananiambia ananipenda,” alisema. 
 
Msami ambaye pia alidai tayari alishadate na mwanadada huyo, alisema anashindwa kuwa karibu na mrembo huyo kwa kuwa tayari alishafunga ndoa na mtu mwingine.
“Kuna vitu vilikuwa vinatokea kwenye mtandao hasa hasa maugomvi. Nikaona jamaa anacomment vitu ambavyo vikuwa vinanihusisha mimi. Mimi nikamwambia Irene sio fair mpigie Hamad haipendezi kuonekana hivi vitu vinakuwa hivi, mimi sivifurahii baada ya hapo nahisi alimwambia,” alisema.

Pia Msami amesema kwa sasa hapendi kujihusisha kwenye mapenzi na staa kwani watamuondoa kwenye njia anayotaka kupita.

0 comments:

Post a Comment