Pages

Subscribe:

Wednesday, January 27, 2016

DIAMOND: SWIZZ BEATZ ANATAKA NIFANYE NAYE KAZI

Producer na Rapper wa Marekani, Swizz beatz hakuishia kuicheza ‘Nana’ na ‘Nataka kulewa’ za Diamond hivi hivi bali anataka kufanya nae kazi. Akiongea na Ayo Tv, Diamond amesema Producer huyo ambaye pia ni Mme wa Alicia keys alimtafuta hivi karibuni kwa lengo la kutaka waingie studio. 

“Kuna Collabo na watu wengi sana Kwa mfano kama juzi, juzi kati nafikiri, kama siku tatu nyuma hivi Swizz alinicheck akanambia itabidi tufanye kazi nikamwambia...
sawa, na tuko tunaplan, nikamwambia mimi nakuja Marekani nafikiri mwezi wa tatu kama sijakosea, au before mwezi wa tatu, kwasababu kushoot video yangu niliyofanya na Neyo, ndio tunaenda kushoot video, Ah nikamwambia nikija ndio itakuwa time nzuri tunafanya hapo hapo” Alielezea Diamond .

Ukaribu wa Diamond na Producer huyo mkongwe wa Marekeni Swizz Beatz ulianza baada ya Producer huyo kupost video mbili tofauti akicheza na mtoto wake nyimbo za Diamond.
Pia Diamond amesema ana collabo nyingine kubwa na msanii wa Marekani japo alikataa kumtaja.

0 comments:

Post a Comment