Maafisa wawili wa Burundi wamekamatwa na kushtakiwa baada ya timu yao kuhusika kumchezea rafu rais wa Burundu, Pierre Nkurunziza katika mchezo wa kirafiki aliyochezwa dhidi ya mkuu huyo wa nchi.
Mtu mmoja akieleza kwa sharti la kutotajwa jina amesema kuwa kiongozi wa timu ya Kiremb, Cyriaque Nkezabahizi na naibu wake ambaye alikuwa msimamizi wa mchezo huo, Michel Mutama wameshitakiwa kwa...
kosa hilo lililofanyika wakati rais Nkurunziza akiichezea timu yake ya Haleluya FC siku ya Alhamisi.
Hayo yote yametokea kipindi ambacho Kiremba FC ilipocheza na timu ya
Haleluya ambayo aliichezea Nkurunziza mwanzoni mwa mwezi huu.
Wakazi wa mji huo wamekiambia chombo cha habari cha AFP
kuwa, Cyriaque Nkezabahizi na mwenzake Michel Mutama waliwaingiza
baadhi ya wachezaji ambao ni wakimbizi kutoka Congo wanaoishi katika
kituo kimoja kilichopo eneo hilo.
Hawa wa Congo hawakumfahamu rais Nkurunziza kwasababu walikuwa wakimchezea rafu wakati wa mchezo huo na kumvamia kila wakati anapokuwa na mpira na kumuangusha.
Rais Nkurunzinza hupenda sana soka na hutumia nusu ya wiki kusafiri
na timu yake ya Haleluya na kwaya yake iitwayo “Komeza gusenga”.
Wakati huo huo hushiriki katika shughuli na miradi mbali mbali ya kijamii na kujionea hali ya maendeleo mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment