Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya uhalifu huo wakitumia...
bisibisi, nyundo na tindo kuvunja nyumba na kuiba vitu kadhaa.
“Tumefanya Operesheni maalum pamoja na misako katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya. Operesheni hii ililenga kukamata wahalifu mbalimbali likiwemo kundi la vijana wanaojiita Wakorea ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.” -Kamanda Mpinga
Kamanda Mpinga amewaambia wanahabari kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa.
0 comments:
Post a Comment