Pages

Subscribe:

Friday, May 1, 2015

WEMA SEPETU: NI KWELI NIMEOLEWA NA TAYARI NI MKE WA MTU

Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu amekiri kufunga ndoa bomani hivi karibuni ambayo ilihudhuliwa na watu wachache. Akizungumza na Clouds FM alisema kuwa aliamua kufunga ndoa ya siri kwa kuogopa kupigwa 'juju' na mumewe angeshindwa kumuoa. ‘’Mume wangu ni Mtanzania na siyo maarufu na ndoa yangu ilihudhuliwa na... ndugu zangu wachache na ndugu wa mume wangu sikutaka watu wengi niliogopa kupigwa juju na mume wangu asingenioa,’’alisema Wema. Hata hivyo alipoulizwa kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba alisema kuwa mumewe amelikubali na hana tatizo Hongera sana Wema

0 comments:

Post a Comment