Pages

Subscribe:

Tuesday, September 6, 2016

BEN POL: MPANGO WANGU WA KUTOA ALBUM MWAKA HUU UPO PALE PALE


13649292_266385900403070_2002980860_n
Ben Pol amedai kuwa mpango wa kutoa album yake mwaka huu upo pale pale. Ameidai kuwa album hiyo imechelewa kutoka kwasababu yeye na uongozi wake wanatengeneza mkakati wa kuipromote na kuiuza ili iende mbali na kumfikia kila shabiki aliyenuiwa.

Hata hivyo muimbaji huyo wa ‘Moyo Mashine’ amedai kuwa lengo la kuitoa si kupata fedha bali ana sababu zingine kuu mbili. “Moja ni kutengeneza ukamilifu wa...
mwanamuziki,” anasema Ben.
 
“Mimi si mtu wa magumashi, kama unataka ukamilifu wa kuitwa mwanamuziki au msanii uliyekamilika, lazima uwe na album,” ameongeza.

“Lakini pili, nataka baadaye biashara ya album ikirudi kuwa stable, ikija kuwa ni deal yaani, niweze kuwa katika watu ambao walithubutu kutoa album licha biashara kuwa bado si nzuri, Ben Pol alikuwepo, kwahiyo niingie kwenye wale wanaharakati waliothubutu kurudisha biashara ya album regardless ya situation ya mauzo ya kipindi hicho au situation ya biashara yenyewe kwa ujumla.”
“Kwahiyo watu wategemee album yangu mwishoni mwa mwaka huu mzigo utatoka.!

0 comments:

Post a Comment