Pages

Subscribe:

Thursday, September 15, 2016

WASANII NA VIONGOZI WA WCB WAALIKWA NYUMBANI KWA RAIS MSTAAFU JK

Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.

JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye ame-support sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao. Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa... kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki.

“Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

0 comments:

Post a Comment