Pages

Subscribe:

Thursday, September 29, 2016

YOUNG KILLER: NGOMA YANGU MPYA INAYO KUJA NI BEST KULIKO

young-killer
Mkali wa kuchana, rapa Young Killer Msodoki amesema ameamua kuwafurahisha mashabiki wa muziki wake kwa kufanya baadhi ya mabadiliko katika nyimbo zake. Akiongea wiki hii, rapa huyo amesema wimbo wake mpya ambao atauchia hivi karibuni utakuwa ni moja kati ya nyimbo zake bora.

“Labda niwaambie kitu kimoja hii ni exclusive, ngoma yangu ambayo nitakuja kuitoa baada ya hii ‘Mtafutaji’ ndo ngoma yangu best kabisa,” alisema Young Killer. Aliongeza,”Sio best kuliko zote zilizopita, lakini hii inayokuja ni best kwa sababu ni ngoma kali kiukwei yaani...
naamini watu watapenda kiukweli. kwa hiyo ubora wake nazungumzia utunzi, jinsi ambavyo style imeifanya, uandishi nimebadilisha, kuna vitu vimekuwa imara zaidi, kwa hiyo mimi nasema mashabiki wangu wakae mkao wa kula,” 

Rapa huyo amesema kabla ya kuachia wimbo huo ataachia kwanza video ya wimbo ‘Mtafutaji’ ambao aliuachia wiki chache zilizopita.

0 comments:

Post a Comment