Pages

Subscribe:

Saturday, September 24, 2016

COUNTRY BOY: KUNA UWEZEKANO WA KUMRUDISHA YOUNG DEE MTU CHEE


14073252_334790183519917_1715470813_n
Rapper Country Boy amedai kuwa kuna uwezekano wa kundi la Mtu Chee kurejea tena likiwa na Young Dee. Mara ya mwisho Young Dee alidai kuwa hawezi kurudi kwenye kundi hilo. Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Country Boy amesema anawasiliana karibu kila siku na Dee.

“Mtu Chee ipo na inarudi upya muda wowote, Young Dee ni mwanetu hatuna matatizo naye, Stamina hana matatizo, mimi sina tatizo, tunajaribu kupiga story kuangalia...
tunafanyaje,” amesema.

Rapper huyo amesema licha ya kutokuwa na uhakika wa kuja na ngoma yao watatu wakiwa pamoja hivi karibuni, amewahakikishia kuwa uwezekano huo ni mkubwa.
Maelezo ya Country Boy yanakinzana na msimamo wa Young Dee kuhusu kundi hilo aliyedai kuwa uamuzi wa kuwaomba arejee kundini kama alivyowahi kushauri Stamina, ‘haumake sense.’

“Mtu Chee mimi pamoja na uongozi wangu sijashauriwa kabisa na sidhani kama kuna siku kutakuwa na hili kundi. Mimi niwatakie kila lakheri katika safari yao ya kimuziki na nawaombea mafanikio huko mbeleni lakini mimi suala la kurudi sidhani kama lipo tena,” alisema kwenye mahojiano miezi miwili iliyopita.

Kauli hiyo ilimfanya Stamina atoe kauli yake iliyoonesha kuwa hazikuwa zikiiva kati yake na rapper huyo wa MDB. “Mtu kama mimi unadhani ninaweza nikababaishwa na sentensi kama hiyo ya yeye kutorudi kwenye group?” alihoji Stamina kwenye mahojiano na Jembe FM ya Mwanza.

“Mimi ni mwanajeshi ambaye ni jeshi la mtu mmoja sifungamani na mtu na wala sitegemei usaidizi wa mtu mimi, mimi naweza nikasurvive mwenyewe na mambo yangu yakaenda vizuri tu. Kwahiyo kauli yake yeye arudi, asirudi sisi walaa, kwanza habari yake nimeiona Bongo5, nisingeiona walaa, kwanza simpigiagi simu, yaani sio mwana kiufupi,anajua mwenyewe mistake zake anazofanyaga. 

Kwasababu sasa hivi anaona amerudi sehemu ile ile, anarudi kwenye yale matapishi aliyokuwa amekula mara ya kwanza, ameona kuwa watu wamekubali kumsaidia tena it’s okay. Halafu mimi si selfish aisee, sababu huyu huyu siku kadhaa tu zilizopita tulikuwa tunaishi naye kitaa vizuri tu na tulikuwa na mipango ya kufanya naye kazi lakini mimi watu wenye dharau sio wanangu kabisa,” alisisitiza Stamina.

“Kwahiyo yeye kwa kauli yake hiyo yeye hajamtetemesha mtu yeyote, nikijisikia kufanya kazi na Country Boy nitafanya naye kama yeye sio tena group. Tena kwa taarifa kama hizi nafurahi kwasababu pia naona group life na kila mtu afanye vitu vyake sababu mimi muziki wangu haufungamani na group kwahiyo I don’t care.”
“Kama jana nimeona kauli yake eti ‘haimake sense’, hell no nigga, yeye ndio hamake sense, halafu asitake watu tuanze kuzungumza kauli zetu za ndani pia, kwasababu mimi battle za mdomo siwezi, ukitaka battle washa mic tubattle.”

0 comments:

Post a Comment