Pages

Subscribe:

Sunday, September 18, 2016

NAH REEL: THE INDUSTR INA PROJECT NYINGI NA BILLNAS

billnas
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa The industry, Nahreel ameweka wazi kuwa label ya The industry ina project nyingi na rapper Billnas anayefanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’. Rapper Billnas hivi karibuni aliwapa taarifa mashabiki wake ujio wa project nyingi kutoka The industry.

Akiongea Jumamosi hii, Nahreel amesema kwa sasa wana kazi nyingi na rapper huyo.
“Yeah Billnas na The Industry kuna kazi nyingi zinakuja, nisingependa kuziweka wazi kwa sasa kwa sababu ni...
mapema,” alisema Nahreel. “Lakini pia wasanii wa label ya The Industry tayari wana kolabo nyingi na wasanii wa kubwa hapa nchini, kwa hiyo naweza sema mambo mazuri yanakuja soon,”

Kwa upande wa Kundi la Navy Kenzo, Nahreel amewataka mashabiki wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kazi mpya za kundi hilo.

0 comments:

Post a Comment