Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Abernego Damiani maarufu kama 'Belle9'
ambaye anatamba na wimbo wake mpya 'Mfalme' ameshangazwa na BASATA
kushindwa kulitambua jina lake na kudai kitendo hicho hakina tofauti na
baba asiyejua majina ya watoto wake.
Belle amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja tokea kwa BASATA kupeleka orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambazo zina...
maudhui ambayo ni kinyume na maadili na Kanuni za Huduma ya Utangazaji ya mwaka 2005.
Katika orodha hiyo wimbo wa tatu ni 'Kibamia' iliyoimbwa na wasanii wawili waliungana na kujiita Rostam ambao ni Stamina pamoja na Roma lakini kwa bahati mbaya jina likaonekana kuandikwa Abernego Damiani a.k.a Roma Mkatoliki.
"Kwa hiyo mimi ni Roma Mkatoliki haya basi 'Tongwe record' baby jei mada yo yo yo. Roma Mkatoliki hii ni sawa na kuwa na Baba ambaye akisikia umekosa ana kuhukumu lakini akiulizwa jina la mwanae anaitwa nani anajiuma uma halafu analitaja jina la mtoto wa jirani ambalo huwa analisikia akiwa anakuja kukuhukumu", amesema Belle.

0 comments:
Post a Comment