Pages

Subscribe:

Tuesday, May 31, 2016

BILL NAS: GODZILLA HAJIAMINI SIIGI CHOCHOTE KUTOKA KWAKE


Bill nass 001
Rapper anaekuja kwa kasi kwenye game ya muziki wa kizazi kipya nchini Bill Nass amekanusha madai kuwa amekua akigeza stayles na aina ya utamkaji wa maneno kutoka kwa  rapper Godzila. Kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha D’Wekend Chart Show cha Clouds Tv weekend hii,Bill Nass alidai kuwa licha ya madai ya Godzila na watu wake karibu kudai kuwa katika nyimbo zake amekua akiiga stayles kutoka kwake, anaamini kuwa hawalingani na hawafanani kwa chochote na...
kuongeza kuwa kaitika nyimbo zake amekua akitumia stayle ya kuimba na kurap huku akichanganya kiswahili na kingereza kama anavyofanya Godzila na kuongeza kuwa kuna utofauti mkubwa sana kati yake na Godzila hasa katika maudhui ya nyimbo zao.

“Niliona post zake,ila sijawahi kupost chochote wala kumjibu coz niliona kama anatupa jiwe gizani….sipendi sana kuzungumzia hiyo issues….naona kama hainifaidishi chochote,namuheshimu Zila kama brother ila anatakiwa ajiamini na afanye mziki wake”alidai Bill Nass.

Alipoulizwa kama huwa anasikiliza nyimbo za Godzila,rapper huyo alijibu “kusikiliza nyimbo haimanishi kwamba ni kali,naweza kusikiliza kwasababu Marcochali kapiga beat kali….ila I get high sio nyimbo mbaya,Nataka sio nyimbo mbaya na ile nyimbo yake ya kwanza ile….inaitwaje ahaamm Get off my way sijui..yeah sio mbaya”alijibu Bill Nass.
 Linner sangaaaa 002
Hata hivyo Bill Nass ambae wiki hii alitambulisha video ya wimbo wake mpya “Chafu Poz”alionekana kutovutiwa na swali na Co-Host wa show hiyo Soudy Brown alietaka afafanue ukaribu wake na mwanamuziki Liner ambae kwa siku za karibuni zilizagaa tetesi kuwa rapper huyo anatoka nae kimapenzi.”She’s good friend of me,she’s suportive hata kwenye wimbo wa Chafu Pozi aliingiza sauti yake kwenye intro”alijibu kwa kifupi.

0 comments:

Post a Comment