Pages

Subscribe:

Tuesday, May 24, 2016

STAMINA NI MSANII HATARI TATIZO NI MANAGEMENT TU

Stamina


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Stamina ni moja kati ya wasanii wa ndani ambao walifanya show kali katika tamasha kubwa la Jembeka Festival 2016 lililofanyika Jumamosi hii katika viwanya vya CCM Kirumba Mwanza.

Katika tamasha hilo, msanii mkali wa Marekani, Ne-Yo alifanya show kubwa ambayo iliwavutia mashabiki wa muziki wa Kanda ya Ziwa.
 
Kati ya wasanii wachache wa ndani waliopanda katika jukwaa la Jembeka Festival 2016 na kuonesha uwezo mkubwa ni Stamina. Alifanya show ya...
kistaarabu huku akiimba nyimbo huku mashabiki wakiimba naye mwanzo mwisho.


Mashabiki wa Jembeka Festival 2016 walionyesha kuelewa na kupenda nyimbo pamoja na style za uchanaji wa Stamina, kwani ulifika wakati wakawa wanafanya chochote wanachoambiwa na rappa huyo.


Shangwe kwenye show za Stamina siyo jambo jipya, kwani show nyingi za Stamina zinakuwa ni kali, labda ni kutokana na kuimba live katika show zake kitu ambacho ni tofauti na wasanii wengine ambao hutumia playback.


“Ahsanteni Mwanza jana kwenye Jembeka Festival 2016. Hamna haja ya picha picha za kuedit za mashabiki, waliokuwepo wanajua nini kilitokea,” aliandika Stamina kupitia instagram yake.


Licha ya mazuri yote anayofanya miaka nenda rudi huku akionekana yupo palepale kimaendeleo, Stamina anahitaji management nzuri ambayo itamsaidia kutimiza malengo yake pamoja na kuufikisha muziki wake mbali zaidi.

Hapa tunazo baadhi ya management kama WCB, Tip Top Connection, QS Mhonda na nyingine nyingi ambazo zimeonyesha jinsi zilivyoweza kuwasaidia baadhi ya wasanii na kuwafikisha sehemu fulani. 


WCB iliweza kumchukua msanii kama Raymond na Harmonize na kuwafanya kuwa wasanii wakubwa ambao wanatambulika ndani ya nchi na nje kwa muda mfupi huku wakiwa na malengo ya kufika mbali zaidi.


Kwa msanii kama Stamina anahitaji kupata uongozi ambao utaendeleza pale alipoishia. Stamina anatakiwa afanyiwe ‘branding’ kubwa pamoja na kuandaa mpango mkakati ya kwenda kimataifa na kutengeneza pesa zaidi.


Muziki ni wakati, tuliwaona akina Mr Nice, Dudu Baya, Juma Nature, Inspector Haroon na wengine ambao walikuwa wakubwa katika kipindi cha nyuma, lakini wakati wao kwa sasa umepita, lakini kwa Stamina huu ni wakati wake sahihi wa kutengenza pesa, kwani ana kila kitu.


Stamina akipata management sahihi, basi atakuwa msanii mkubwa sana kutokana jinsi mashabiki wanavyomchukulia na kumuelewa.

0 comments:

Post a Comment