Pages

Subscribe:

Tuesday, May 31, 2016

MTOTO WAKIUME AZALIWA AKIWA NA NYWELE SEHEMU ZA SIRI NA HAMU YA NGONO

34C56F6700000578-3616389-The_toddler_known_only_as_Akash_was_found_to_have_the_testostero-a-22_1464615966532


Mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja nchini India aliyebainika kuwa na nywele kwenye sehemu zake za siri na hamu ya kufanya mapenzi amegundulika kuwa na tatizo la homoni ambalo ni nadra sana.

Mtoto huyo ambaye jina lake ni Akash, alipatikana akiwa na homoni za testosterone zenye kiwango cha mtu mzima mwenye miaka 25. Hiyo inamaanisha kuwa alikuwa na uume wenye size kama ya mtu mzima, ndevu na nywele za sehemu za siri pamoja na...
sauti isiyoendana na umri wake.

Madaktari sasa wanadai kuwa mtoto huyo ana tatizo liitwalo precocious puberty ambapo mtoto hubalehe kabla ya miaka saba au nane.

Wazazi wa Akash mwanzoni waligundua kuwa kuna kitu hakipo sawa kwa mtoto wao alipokuwa na miezi sita. Uume wake ulikuwa ukiwa mkubwa kuliko kawaida, wakati mwili wake ulikuwa mdogo mno ukilinganisha na watoto wa umri wake.

“Tulidhani labda alikuwa mtoto mkubwa, hivyo hatukumpeleka kwa daktari,” mama wa mtoto huyo aliliambia gazeti la Hindustan Times.
“Lakini alipofikisha mwaka mmoja, ilikuwa wazi kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Mama mkwe wangu, ambaye amewalea watoto kadhaa kwenye familia pia alisema ukuaji wake haukuwa wa asili. Hapo ndipo tulipompeleka kwa daktari.’

Daktari wa Akash, Vaishakhi Rustagi, ameliambia Hindustan Times kuwa tatizo hilo lina athari kwa mtoto na kwamba itafika muda atashindwa kukua na kumfanya awe na urefu wa futi 3-4 muda wote. Mtoto huyo kwa sasa anapewa matibabu.

Precocious puberty ni tatizo la nadra sana. msichana aliyewahi kuzaa akiwa na umri mdogo zaidi kuwahi kutokea ni Lina Medina, aliyezaa akiwa na umri wa miaka mitano na miezi saba huko Peru mwaka 1939, na kuwa maarufu duniani enzi hizo.
28 
Wazazi wake walidhani kukua kwa tumbo lake kulitokana na uvimbe lakini baada ya tiba za mwanzo kutofanikiwa ndipo walipompeleka hospitali.Mwezi mmoja tu baadaye aliushangaza ulimwengu baada ya kujifungua mtoto wa kiume.


0 comments:

Post a Comment