Pages

Subscribe:

Tuesday, May 31, 2016

NAMELESS AAMUA KUUPIGA CHINI MUZIKI

13
Mwanamuziki aliyejitengenezea jina kubwa katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki aliyesifika na Ngoma ya Sinzia, David Mathenge ‘Nameless’ imevuja kuwa amepiga chini masuala ya muziki na badala yake ameamua kudili zaidi na ishu zake zingine za kibiashara.

Kikichonga na gazeti hili, chanzo cha kuaminika kutoka nchini Kenya ambacho kipo karibu na Nameless kilisema kuwa, msanii huyo kwa sasa hafanyi muziki ‘sereousy’ kama...
kipindi cha nyuma na zaidi anajishughulisha na uchoraji wa ramani za majengo kazi ambayo inamuingizia mtonyo zaidi.

“Nameless kwa sasa amehamishia nguvu zake kwenye biashara ya kuuza ramani za majengo, huko anapiga mtonyo zaidi na hata akisikika kwenye ngoma ni vile muziki ni sehemu yake lakini si kwamba anaendelea na biashara hiyo,” kilisema chanzo hicho.

0 comments:

Post a Comment