Pages

Subscribe:

Wednesday, May 25, 2016

WEMA SEPETU: IPO SIKU NTAITWA MAMA

Wema Sepetu ana kila kitu anachokitaka duniani, fedha, magari na vingine lakini amekosa kitu kimoja tu muhimu – mtoto.

Na Miss Tanzania huyo wa zamani anataka watu wajue kuwa suala la mtoto si kitu anachokichukulia poa hata kidogo. Muigizaji huyo alielezea hisia zake hizo kwa kupost picha akiwa na mama yake na kuandika: Iko siku na mimi ntaitwa Mama.’ Aliongeza... emoji za mtu mwenye huzuni.

Miezi kadhaa iliyopita Wema na Idris walitangaza kutarajia kupata watoto mapacha lakini baadaye walitangaza kuwapoteza. Kwa muda mrefu Wema amekuwa muwazi kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba katika muda anaotaka kufanya hivyo.

Mashabiki wake wameendelea kumpa moyo na kumtaka asikate tamaa.

“Usikate tamaa @wemasepetu unakumbuka sara wa ibrahim alizaa akiwa mzee sana cha msingi endelea kumwomba mungu na jiweke karbu nae hakuna kinachoshindikana kwake,” ameandika shabiki mmoja.

0 comments:

Post a Comment