Pages

Subscribe:

Tuesday, May 31, 2016

MASIMANGO YALINIFANYA NIMTAFUTE BABA YANGU

Msanii Gerry wa Rhymes amefunguka kuhusu sababu iliyomfanya amfuate baba yake mkoani Shinyanga, na kuonana naye kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 kupita, tangu waonane kwa mara ya mwisho. Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Gerry amesema masimango aliyokuwa akiyatoa baba yake wa kambo pamoja na kitendo cha...
kupata mtoto, kilimfanya aende akamtafute baba yake mzazi.

"Unajua mi wazazi wangu walizinguana, sasa nikawa na bi mkubwa, sasa yale maneno ya baba wa kambo kwamba aende kwa baba yake.. sijui ana baba yake..ilikuwa inaniumiza, na pia sasa hivi ni baba, mtoto wangu ana miaka minne anaenda mitano, na mtoto wangu ananipenda sana, nikaona hii love ambayo ananipa huyu dogo kwa nini na mimi nisimtafute mshua wangu!? hata kama walizinguana, nikamtafuta alikuwa mkoani Shinyanga, nikaenda nikameet nae", alisema Gerry.

Pia Gerry aliendelea kusimulia tukio hilo ambalo ni kubwa katika maisha yake, na kulezea siku alipoonana naye, na jinsi baba yake huyo alivyompokea baada ya miaka 21 bila kutiana machoni.
"Cha kushangaza ni kwamba mwana hajashtuka kabisa kwamba mtu hajaonana na mwanaye miaka mirefu, yani aliponiona as if tumetoka kuonana masaa matatu yaliyopita, yani mshua alikuwa hana habari lakini all good, nimemuona nimeshkuru maisha yanaendelea", alisema Gerry wa Rhymes.

0 comments:

Post a Comment