Pages

Subscribe:

Saturday, February 14, 2015

MAFUTA YA KULA YENYE THAMANI YA Tsh MIL 34 YAKAMATWA BANDARI YA TANGA

 
Shehena ya mafuta ya kula zaidi ya madumu 888 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 34 kutoka Singapore yamekamatwa katika bandari bubu ya Kwale iliyopo pembeni mwa bahari ya hindi yaliyokuwa yakitokea kisiwani Zanzibar kwenda jijini Tanga bila kulipiwa ushuru. Kukamatwa kwa mafuta hayo kunafuatia operesheni inayofanywa na askari wa kikosi cha...
wana maji katika bahari ya Hindi ambapo imebainika kuwepo kwa bandari bubu 280 katika wilaya za Mkinga, Tanga, Muheza na Pangani ambapo kati ya hizo 40 ni kubwa na nyingine ndogo ambazo zinatumika kuingiza bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kukwepa ushuru unaotozwa na watendaji wa serikali.
Kufuatia jitihada hizo wasemaji wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga wamesema mtuhumiwa aliyedaiwa kukwepa kodi kwa serikali atalipa kodi kisha atatozwa faini kulingana na shehena ya bidhaa zilizokamatwa hivyo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo katika kufichua wakwepa kodi na endapo zoezi hilo litafanikiwa watatoa donge nono kwa mhusika.
Hata ivyo nahodha wa jahazi lililokutwa likisafirisha bidhaa hiyo Ally Rashid amesema kilichosababisha chombo chao kuweka nanga katika bandari bubu ya Kwale ilitokana na kupasuka kwa tanga linaloongoza safari pamoja na kuharibika kwa mashine hatua ambayo imewalazimu kukaa siku Tisa majini na kujikuta wakisogezwa hadi bandari bubu ya kwale.

0 comments:

Post a Comment