Pages

Subscribe:

Saturday, February 28, 2015

BEN POL: KIUKWELI WANAIJERIA HAWATUWEZI KIMUZIKI

Msanii Ben Pol ambae kwa sasa anafanya poa na kazi yake mpya ya Sophia amefunguka na kusema kuwa wasanii wa Nigeria hawawawezi wasanii wa bongo kwa kipaji na kutengeneza ngoma kali na hilo amelithibitisha msanii Diamond Platnum ambae kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Nitampata wapi ambao unaoneka kufanya vizuri zaidi kuliko hata ngoma za wasanii wa Nigeria katika baadhi ya vituo vya habari ndani na nje ya Tanzania. Ben Pol amesema hayo kupitia... Account yake ya Twitter ambapo amesema msanii Diamond kishamfunga paka kengele na kilichobaki ni kuongeza nguvu na kuona ni jinsi gani wanaweza kupenya zaidi na kuzidi kutanua mipaka ya Bongo fleva ulimwenguni.
"Kiukweli Wanigeria Hawatuwezi Kimuziki,Na kuhusu Nani Atamfunga Paka kengele, Tayari Diamond Ameshamfunga Paka kengele"
Ben Pol amekuwa msaniii wa pili kuonyesha kuwa muziki wa Bongo fleva ni muziki mzuri kuliko muziki wa Nigeria kwani hata msanii Mwanafalsafa alishasema kuwa haupendi na haukubali kabisaa muziki wa Nigeria.Licha ya baadhi ya wasanii kuusujudu na kuamini ndiyo muziki mzuri na ambao wanahisi unapendwa sana kwa sasa lakini kwa Mwana Fa imekuwa tofauti kwani alisema "Katika Habari nyingine,nimeamua kuwa hater wa mziki wa Nigeria".
Kwa upande wake Diamond amezidi kushukuru Mungu kuona wimbo wake huo wa Nitampata wapi unazdi kuchana mawimbi na kupokelewa vizuri hata nje ya Afrika Mashariki kitu ambacho kinamfanya kujiona ni balozi mzuri zaidi wa Afrika Mashariki.
"Asante Sana Mwenyez Mungu kwa Baraka zako zinazonifanya nizidi kuiwakilisha vyema Nchi yangu na Afrika Mashariki yangu..."

0 comments:

Post a Comment