Pages

Subscribe:

Thursday, February 19, 2015

OMMY DIMPOZ AMKANA WEMA SEPETU


Msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema anashangazwa na uvumi unaoendelea kuwa yupo katika uhusiano na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu. Akielezea kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandano ya kijamii, Ommy Dimpoz, alisema walikuwa Afrika Kusini kwa... mapumziko ndipo picha hizo zilipopigwa.

“Tunapiga picha nyingi sana na Wema hata uki-google utaziona, hii siyo mara ya kwanza, lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki,” alisema.

Ommy alisisitiza kuwa yeye hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ex wa rafiki yake, na kuwa yeye na Wema walikuwa wakifahamiana hata kabla ya Wema kuanza mahusia ya kimapenzi na Diamond. Hivyo kuacha kwao haiwezi kumpelekea yeye awe mbali nao kwani hayo ni mambo yao binafsi.

Japokuwa Ommy anaamni kuwa kwenye pitapita za kimaisha inawezekana mtu akawa na mahusiano ya kimapenzui na Ex wa rafiki yake, kwani hicho kitu kinawezekana.

“Ku-date na Ex wa rafiki yangu, kwa mimi hapana lakini kuhusu maswala ya mapenzi lolote linaweza kutokea kwasababu umesha sema Ex kwahiyo it means hawapo kwenye mahusiono tena kwahiyo inaweza ikatokea huko mbele mbele maisha yameendelea  watu wakaja kukutana , kwa huyo vitu hivyo vinawezekana”  Dimpoz alieleza.

Picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu aliyonao Ommy Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema, Nasib abdul ‘Diamond’

0 comments:

Post a Comment