Pages

Subscribe:

Thursday, February 19, 2015

RICH MAVOKO ALAMBA DILI LA UBALOZI WA WWF

Hit maker wa "Mapacha" Rich Mavoko apata shavu la kuwa balozi wa shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa mazingira, World Wide Fund (WWF) kwa mwaka mzima. Dili hilo embalo amelipata baada yakushoot video ya wimbo wake mpya "Mapacha"nchini South Africa, ambapo anaonekana akiwa anaimba na mnyama Duma akiwa pembeni yake. Mavoko amezungumzia jinsi... video hiyo ilivyopelekea kumpa shavu hilo kwa kusema..

"Waliangalia video yangu "Pacha Wangu", nilivyomtumia Chui walipenda na kuvutiwa na mimi," amesema Mavoko
"Walipenda kufanya kazi na kijana ili niweze kuwashawishi vijana wenzangu kutunza mazingira." alimaliza kusema 
Mavoko amechaguliwa kuwa balozi ambae atasimamia mradi wa solar for education kuhakikisha shule zozote za vijijini zinatumia umeme wa nishati ya jua.
"WWF ni shirika linalojihusisha na utunzajiw a mazingira, na mimi nimechaguliwa kuwa kama balozi pale kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kushawishi watu wasikate miti na kuwashauri kutumia nishati ya jua, hizi sola hizi. Kuna baadhi ya shule tutaenda kugawa, shule za pwani maeneo ya kisarawe tutaenda kugawa solar kwa shule zitakazo andika insha vizuri, kwahiyo watakaoshinda mi ntakuwa kama mgawaji pale.... amesema Rich Mavoko

0 comments:

Post a Comment