Pages

Subscribe:

Tuesday, February 24, 2015

SARMY CLEVER: SIHITAJI KUKURUPUKA NATAKA KUFANYA KITU KILICHO BORA ZAIDI


Baada ya kuona wimbo unahit sana ktk redio mbali mbali kwa muda huku masabiki wakiwa na hamu kubwa ya kuona na video ya ngoma ya Tausi iliyoimbwa na mkali wa Bongo Fleva Samry Clever hatimaye msanii huyu afunguka na kukata kiu ya mashabiki wanaotaka kuona video ya ngoma hiyo.
Bila kuchelewa tulimtafuta Sarmy na kukaa naye kisha tukazungumza mawili matatu kuhusiana na swala hili Sarmy alisema..
amekisikia kilio cha mashabiki zake na wasiwe na wasiwasi kwani hataki kukurupuka yupo anajipanga ili aweze kutoa kitu kilicho bora pia alionesha mfano juu ya swala hili sarmy alisema angalia video za watu kama Madee, Temba na Chege nyimbo zao ni zakawaida lakini ukali wa video zao umefanya nyimbo zionekane bora.

Hivyo mashabiki zangu wasiwe na wasiwasi najiandaa kuwaletea kitu kilicho bora na sihitaji kukurupuka kwani ntachekesha jamii. Alisema Sarmy Clever

0 comments:

Post a Comment