Pages

Subscribe:

Monday, March 30, 2015

BABU TALE AFUNGUKA KUHUSU KIFO CHA KAKA YAKE ABDUL BONGE

Kifo cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul  Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, juzi jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini.

Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge... akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.

Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
"Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo" – Babu Tale.

Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.

0 comments:

Post a Comment