Pages

Subscribe:

Sunday, March 29, 2015

JAY DEE AWEKA WAZI KUWA YEYE NI TEAM KIBA

Kutoka kwenye Account ya Instagram, Mwanadada Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee (Komando Jide) ameamua kutangaza rasmi yeye ni shabiki wa msanii Ali Kiba. Hii inakuja mara baada ya Ali Kiba kumsupport Jide jana usiku katika show yake bila masharti yeyote huku Ali Kiba akipata shangwe kali kutoka kwa mashabiki.. Lady jay Dee kaandika hivi...
..Mdogo wangu Ali Kiba
Natoa shukrani zangu za pekee kwako
Asante kwa kuteka show..
Sina cha kuelezea
Halikuwa funiko lile, bali
Labda niseme lilikuwa ni Zege
Unajua nini maana ya Shukrani ....
Sijawahi kukutendea makubwa ya ajabu
Ila tendo la kuamua ku support ur sister
Bila kuniwekea masharti
Ni upendo tosha
Inatosha ❤
Wengi wanaogopa
Ila umesimama
Na kuona umuhimu wangu kwako.
Katika kipindi kigumu nilichopo. I will forever love you
Keep the fire burning.
Nilikuwa
Na nitaendelea kuwa ✔
Natangaza rasmi kuwa
Mimi ni #TeamKiba
Now & Forever
Kama wewe ni TeamJide ... na bado hujawa' .... badi usisite kuwa Team Kiba
Oyoooooooooo ......
#FunikaMbaya
Next tukafanyie uwanjani sio ishu..

0 comments:

Post a Comment