Pages

Subscribe:

Tuesday, March 10, 2015

KAULI YA MAMA MARIA NYERERE BAADA YA KUZUSHIWA KIFO

Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jana  jioni  alizungumza na kituo cha runinga cha Taifa, TBC na kukanusha uvumi ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameaga dunia. Akizungumza na mtangazaji, Mama Nyerere alimuuliza... "ukiniangalia unanionaje?" ambapo mtangazaji alimjibu, "nakuona mzima!" huku wakitabasamu.

Mama Maria alisema huu ni mwaka wa uchauguzi, hivyo mambo haya ya uzushi si ya ajabu.

Kabla ya uvumi wa kizushi kuhusu Mama Maria, juzi kupitia WhatsApp ulikuwa ukitumwa ujumbe mwingine wa kumzushia kifo Reginald Mengi, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP.

0 comments:

Post a Comment