Pages

Subscribe:

Monday, March 16, 2015

SARMY CLEVER AWAJIA JUU WAGANGA BAADA YA MAUAJI YA WALEMAVU WA NGOZI KUKITHIRI


Kumekuwa na stori nyingi za wasanii kujihusisha na maswala ya ushirikina kutumia waganga ili waweze kufanikiwa katika maswala yao ya kimuziki na wengi wao wamekuwa wakitumia waganga kwa kisingizio cha kusema kuwa walienda kujikinga na kusafisha nyota zao, Na imeonekana kuwa waganga ndiyo chanzo kikubwa kinacho pelekea walemavu wa ngozi (Albino) kutoishi kwa amani ktk ardhi ya nchi yao wenyewe.

Mwandishi aliamua kumtafuta mmoja kati ya wasanii wa hapa bongo anaye julikana kama Sarmy Clever na kuzungumza naye juu ya maswala ya ushirikina ktk sanaa ya muziki Sarmy alisema..
Kiukweli siwezi kusema kuwa ushirikina haupo kwani nafsi za watu zinatofautiana huwezi jua nafsi ya mtu mwingine anacho kifanya kwakweli ushirikina upo tena saana tu, ila kwa upande wangu sijawai kwenda kwa mganga mi namwamini sana allah ndo maana naswali kila ijumaaa, Na pia alipo ulizwa juu ya mauwaji ya albino Sarmy alisema kama kweli waganga wanahusika basi waachane na mchezo huo.

Mwandishi: Je unahisi ni adhabu gani wanastahili kupewa hawa wahusika wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi?
Sarmy: Mi adhabu ninayoona wapewe kama Ameua nayeye auwawe Kama kamkata mkono nae akatwe hivyo hivyo adhabu iendane na kosa. Alisema Sarmy Clever

0 comments:

Post a Comment