Pages

Subscribe:

Saturday, March 14, 2015

KNOW MORE ABOUT SARMY CLEVER THE TANZANIAN MUSICIAN ARTIST


Mussa Mohamed Amry "Sarmy Clever" (Amezaliwa 17.08.1993). Ni msanii kutoka Tanzania wa Muziki wa kizazi kipya aina ya Bongo Fleva, anauwezo wa kuimba, Kuigiza, Kuchekesha, Sarakasi, Kucheza mpira na pia ni mchezaji mzuri wa mchezo wa Kungfu. Alizaliwa ktk Hospitali ya Meta iliyopo jijini Mbeya na baada ya kupita miaka kadhaa wazazi wake walitengana hivyo ikabidi Sarmy alelewe na...
ndugu za wazazi wake, hivyo aliishi mikoa tofauti tofauti ikiwemo Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro na Mbeya. Alichukuliwa na kulelewa ma mama yake baada ya ndugu aliokuwa akiishi nao kumpa mateso makali, Alisoma Miganga Secondary na Kumalizia elimu yake Mwenge High School.

MAISHA YA MUZIKI:

Mbali na kuwa na vipaji vingi Sarmy alikuwa anapenda sana kuimba na ndoto yake kubwa ilikuwa  kwamba siku moja naye aje aingie Studio hivyo Sarmy alikaa chini na kuanza kutunga nyimbo na wimbo wake wa kwanza uliitwa NI WEWE ilipofika tarehe 24.08.2014 Sarmy aliingia rasmi Studio na kufanya wimbo huo ambao alimshirikisha kijana mmoja aliye julikana kwa jina na Maru, Wimbo huu ulifanywa na Producer Zest lakini wimbo huo ulipo toka Sarmy hakuupenda wimbo huo kutokana na producer kutoipenda kazi yake ( Wimbo ulikuwa chini ya kiwango), Baada ya muda Sarmy ilimbidi akaurudie tena wimbo huo kwa mara ya pili na wakati huo ilibidi akaifanye kwa producer mwingine aliye julikana kwa jina la  Berry K na baada ya hapo wimbo ukaachiliwa rasmi. Wimbo NI WEWE haukuweza kuwa hit sana kwa sababu Sarmy alikosa sapoti ya kutosha kwa kuwa ndiyo kwanza alikuwa anaanza.

Mwishoni mwa mwaka 2014 sarmy Clever aliingia tena Studio kwa mara nyingine tena na wakati huu alikuwa amekuja na Aidia nyingine tena ya winbo mwingine na wakati huu alirekodi wimbo mpya uliokwenda kwa jina la TAUSI, Wimbo huu ndiyo wimbo ulio mtambulisha msanii huyu ktk maisha yake ya muziki kwani baada ya kuuachia wimbo huu wa TAUSI ulisambaa kwa haraka kutokana na wimbo huu kuweza kupewa ushirikiano wa kutosha. Kama unavyo jua sikuzote katika maisha nguvu kubwa ipo kwa wanawake basi wimbo wa TAUSI ulipendwa sana na watoto wa kike na hicho ndiyo chanzo cha wimbo huu kuweza kusikilizwa sana kuliko wimbo wa kwanza Kwa ufupi TAUSI ndiyo wimbo ulio mtambulisha ktk sanaa ya muziki.

Wimbo TAUSI ulimfanya Sarmy kupata show nyingi na mikoa mbali mbali na show yake kubwa ya kwanza lifanya mkoani Iringa. Show hiyo ilihusisha wasanii mali mbali lakini akiwemo msanii mkubwa Tanzania na Africakwa ujumla ( Diamond Platinumz). Kama unavyo jua kila kitu huwa kinakuwa na kishawishi hivyo pamoja na kuwa na kipaji lakini Sarmy Clever alipata ushawishi mkubwa wa kujikita kwenye muziki kutoka kwa msanii MB DOG, DIAMOND na CHRIS BROWN hawa ndiyo wasanii ambao walimvuta huyu jamaa mpaka akajikita ktk muziki kutokana na kuzipenda nyimbo zao naye akajikuta akitamani siku moja aje kuwa kama wao.


AINA YA MUZIKI:
Kama tunavyo jua hapa duniani kuna aina mbali mbali za muziki na kila msanii huwa anastaili yake ya muziki ambao anaimba. Sarmy Clever anauwezo wa kuimba Zouk, R & B, Afropop na Mduara hiyo ndiyo listi nzima ya aina ya muziki anaoweza kuimba msanii huyu.

MAISHA YA KAWAIDA:
Ukitoka nje ya muziki sasa tukija ktk maisha yake ya kawaida sasa msanii huyu shughuli anayo fanya ni Mwajiriwa ktk kampuni moja ya kubwa ya simu hapa nchini, Sarmy Clever anaurefu wa 170CM

JINA SARMY CLEVER:
Kama ulivyo soma hapo mwanzo kuwa Jina Sarmy Clever ni jina la kupachikwa tu lakini jina lake halisi ni Mussa Mohamed Amry, Jina sarmy Clever lilitokana na Binti mmoja mwenye asili ya kihindi ambaye alikuwani rafiki wa karibu sana wa Msanii huyu ambaye kwa madai yake anasema kuwa binti huyo wakihindi alikuwa akimwita SARMY na jina Clever lilitoka kwa Producer wa msanii huyo baada ya kuona kuwa msanii huyu ana maono au uwezo wa kuona mbali baasi akawa anamwita Sarmy na mbele ya jina Sarmy akawa anaongeza neno Clever kutokana na uwezo wa msanii huyu hivyo jina likawa ni SARMY CLEVER.

SITO SAHAU:
Kila mtu ana historia yake ya maisha Visa na Mikasa aliyo wahi kukutana nayo na kuna mambo ambayo katika maisha mtu hawezi kuja kusahau mpaka umauti unapo mkuta, Hivyo msanii Sarmy Clever alipoulizwa na mwandishi kuwa ni jambo gani ambali huwa linamuumiza kila anapo likumbuka na hato kuja kulisahau ktk maisha yake Sarmy alisema:

JAMBO NISILO KUJA KULISAHAU: kutengana kwa wazazi wangu nikiwa mdogo sana na kutokuishi nao na kuishi kwa ndugu walinitesa sana walinipiga sana mpaka mwili wangu kujenga sugu na vidonda,kulala njaa,kiufupi sijafaidi malezi ya wazazi wawili mama baadae ndiyo alinichukua na kunilea kwa uangalifu nampenda sana mama.

3 comments:

Unknown said...

pole kaka na mwenyezi mungu atakusaidia sanaaaaa

Unknown said...

na mimi najua wewe unajua nautakuja kuwa kiboko yao soon

Unknown said...

dahhhh nakuombea sanaaaaaaaaaa

Post a Comment