Pages

Subscribe:

Friday, March 13, 2015

OMMY DIMPOZ: DIAMOND SI YUPO NA ZARI? HAWEZI TENA AKAWA FOCUS NA WEMA

Mwanamziki Ommy Dimpoz ameyasema hay oleo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga picha za kuutangaza wimbo huo. Ommy alisema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika... chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.

 “Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”

0 comments:

Post a Comment