Pages

Subscribe:

Saturday, February 20, 2016

HAWA NDIYO WACHEZAJI WA SIMBA WANAO KUMBUKWA MUDA WOTE

 Kikosi bora cha Simba cha muda wote
Wamepita wachezaji wengi ktkt timu ya Simba Sports Club tangu ianzishwe ila leo Smashkilimanjaro inakuletea Kikosi Bora cha muda wote cha Simba. Ntakutajia jina la mchezaji na historia yake ktk Club ya Simba.

1.Mohammed Mwameja
Alikuwa kipa tegemeo kwa kipindi chake cha uchezaji kiasi cha kuitwa Tanzania One, huyu ndiyo kipa aliyeifikisha Simba fainali ya CAF, mwaka 1993 na kufungwa na...
Stella Atowar katika mchezo wa marudiano wa fainali.
2.Kombo Aboubakar
Beki wa kulia aliyefanya kazi kubwa na kuingarisha timu hiyo akitokea Sigara, uwezo na kipaji alichokuwa nacho ilisababisha kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ingawa baadaye aliihama timu hiyo na kutua kwa wapinzani wao Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000.

3.Alphonce Modest
Huyu ni mlinzi wa kushoto wa Simba ambaye hadi leo anakumbukwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa kipindi anacheza aliweza kuwadhibiti washambuliaji wakati wa kipindi hicho akiwemo winga wa Yanga Edibili Lunyamila.

4.Athuman Maulid
Mashabiki wengi wa Simba wa miaka ya hivi karibuni nivigumu kumfahamu Maulid, lakini ni moja ya beki mwenye roho ngumu na aliyeitumikia Simba na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo kuibebesha mataji matatu ya ligi daraja la kwanza wakati huo ikiwa ndiyo ligi kubwa nchini.

5.Frank Kasanga (Bwalya)
Huyu naye siyo maharufu sana kwa mashabiki wa Simba hivi sasa lakini ni mmoja ya nembo ya klabu ya Simba kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kipindi chake wakati anaichezea timu hiyo na ndiyo sababu ameingia kwenye kikosi bora cha wachezaji 11 wa muda wote wa klabu hiyo.

6.Ramadhan Lenny
Kiungo mardadi wa Simba aliyepata kufanya vizuri na kujizolea mashabiki wengi katika soka la Tanzania Lenny, alifanya kazi kubwa ya kuipigania Simba na kuchangia mafanikio mengi ikiwemo ubingwa wa Kombe la Kagame pamoja na ule wa muungano miaka ya 1990.

7.Steven Mapunda
Winga hatari kabisa aliyepata kutokea kwenye klabu hiyo kongwe nchini Mapunda alikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilicho ivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri mwaka 2003 licha ya hivyo lakini pia aliweza kuisaidia timu hiy kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani.

8.Adolph Kondo
Huyu ni kiungo ambaye alifanya vizuri katika kipindi chake cha kuitumikia klabu ya Simba na kuisaidia katika michuano mbalimbali iliyoshiriki timu hiyo moja ya mafanikio hayo ni kuipa ubingwa wa muungano kwa kuwafunga watani zao Yanga.

9.Edward Chumila
Mshambuliaji hatari kuwahi kutokea nchini akichukua nafasi za Damiani Kimti waliofanya vizuri kipindi chao, Chumila alisifika kutokana na kupasia nyavu hasa alipokutana na wapinzani wao Yanga.

10.Zamoyoni Mogella
Mshambuliaji wa kati wa Simba ambaye naye alijizolea umaarufu mkubwa kipindi chake na kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo ambayo hivi sasa inapambana kurudi kwenye ubora wake kama ilivyokuwa kipindi hicho.

11.Kipese Thomas
Winga wa kushoto mwenye mbio na chenga za maudhi kwa mabeki wa timu pinzani Kipese aliisaidia sana Simba hata timu hiyo kunyakua taji la Tanzania mara mbili mfululizo na kuwapiku wapinzani wao Yanga miaka ya 90.

0 comments:

Post a Comment