Pages

Subscribe:

Saturday, February 27, 2016

DOGO JANJA: NILIKUWA NAWAZA NTARUDI VIPI


Msanii Dogo janja amesema aina ya muziki anayoifanya sasa hakutarajia kuifanya, kwani alikuwa hajajiandaa kufanya hivyo, lakini ilipotokea mashabiki wake wameonekana kuikubali. Dogo janja ameyasema hayo alipokuwa akiongea na East Africa Radio, na kusema kuwa kabla hajatoa wimbo wake huo mpya alikuwa ana wasi wasi iwapo atafanikiwa kufanya poa, na alikuwa anafikiria ni jinsi gani arudi kwenye game

“Kitu ambacho kilinafnya nichange style, nilikuwa nafikiria jinsi ya kurudi, pia nilikuwa muoga, nikawa narekodi napeleka, narekodi napeleka, kuna jamaa anaitwa Cal kutoka Norway ni producer alikuja...
bongo, sasa walikuwa wamenitumia beat, nikaenda studio nikajikuta nimepata melody, michano, nikawatumia michano management yangu wakaona hii inabidi tuiboreshe, ndio ngoma ikatoka”, alisema Dogo janja.
Pamoja na hayo Dogo janja amesema kubadilika huko hakujamuharibia sana, na watu wakae mkao wa kula upata video yake ambayo iko tayari, na imetengenezwa na Hanscana.

“Nashukuru sijakutana na changamoto kwani hata watu wananiambia huu ndio muziki wako unakufit, ngoma ina video nimeshoot na hanscana, watu watarajie video mpya na Dogo janja mpya”, alisema Dogo Janja.

0 comments:

Post a Comment