Pages

Subscribe:

Saturday, February 27, 2016

PESA ALIZOVUNA MR NICE MIAKA YA NYUMA ZAANZA KUFANYA KAZI

Msanii mkongwe na mwanzilishi ya style ya TAKEU, Mr Nice amefunguka kwa kusema kuwa bado yupo vizuri kiuchumi tofauti na watu wanavyodhani kwamba amefilisika.

Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema kwa kuthibitisha hilo amejenga nyumba mpya kubwa nyumbani kwao ndani ya miezi mitatu.
“Watu hawajui kwamba walinipa pesa nyingi sana mpaka leo bado nazitumia, nyie mnaona kama zimeisha hazijaisha, hapa sasa hivi nawazima kidomo domo wale... waliosema nimefilisika, sasa hivi najenga nyumba nyingine kijijini kwangu Moshi na ndani ya miezi mitatu nyumba kubwa imekamilika,” alisema Mr Nice.

Aliongeza, “Watu ambao umefilisika watafikiria kujenga sasa hivi?, hamuwaoni wasanii wenye stress za maisha, kwa hiyo hili ni jibu kwa wale waliyokuwa wanaongea sana,”

0 comments:

Post a Comment