Pages

Subscribe:

Saturday, February 20, 2016

HII NDIYO SABABU ILIYO MFANYA YOUNG KILLER KUTAKA KUFUNGA NDOA

Young Killer na Halimaty

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Young Killer Msodoki amesema anaamini akifunga ndoa mambo yake mengi katika maisha yatafunguka.

Rapa huyo ambaye ameachia video ya wimbo ‘Popote’ akiwa amemshirikisha Juma Nature, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa, tayari yeye na mchumba wake wamechunguzana na wameona wapo tayari kuanza maisha ya ndoa.

“Siwezi sema tunafunga lini ndoa, lakini muda wowote tunafunga ndoa,” alisema Young Killer. “Unajua ukifunga ndoa kuna... mambo mengi yanabadilika kwenye maisha, Mungu anafungua milango ya ridhiki, yaani kwa ufupi unapata neema fulani. Mimi na Halimaty tunajuana vizuri, hatujakurupuka kusema hivyo.,” aliongeza Young Killer.

0 comments:

Post a Comment