Pages

Subscribe:

Saturday, February 20, 2016

DOGO JANJA AZUNGUMZIA UHUSIANO WAKE NA UONGOZI WA TIP TOP KWA SASA

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Dogo Janja baada ya kusambaa audio yenye sauti yake katika mitandao ya kijamii akidai uongozi wake Tip Top Connetion unambania, amefunguka na kueza hali ilivyo. Rapa huyo ambaye hajatoa ngoma yoyote kwa kipindi cha mwaka mmoja, ameiambia Bongo5 kuwa amejaribu kumtafuta bosi wake Madee ili amweleze kwanini aliongea vile lakini... bado hajampata.

“Kiukweli siwezi kukataa ile sauti ni yangu, na aliyezingua ni msichana na sijui alinirekodi kwa nia gani,” alisema Dogo Janja.
“Mpaka sasa hivi sijaweza kuongea na Madee, nimekuwa nikimtafuta kwenye simu lakini amekuwa hapokei simu zangu, pia nimejaribu kumtumia meseji hajibu. Kama jana tulipata bahati ya kwenda kwa Mh Magufuli na yeye pia nilimuona, lakini sikuweza ongea nae, nilivyosema nimtafute kusema kweli akawa ameshaondoka na sikuweza kumfuta wakati waheshimiwa wako pale ningeonekana msumbufu. Siwezi sema ameichukilije kauli yangu mpaka nipokutana ane ndipo nitazungumza,” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment