Pages

Subscribe:

Saturday, February 27, 2016

NAY: MUZIKI WA SASA SIYO UWEZO ILA NI UJANJA UJANJA

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema muziki wa sasa hivi ukileta ufundi na kujifanya unaweza sana kuchana na kuandika hautafika popote. Nay wa Mitego amedai ili kwenda kibiashara msanii unatakiwa kubadilika ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko. “Muziki wa kipindi cha nyuma ulikuwa wa serious sana, ulikuwa unahitaji uumize sana kichwa ili ufanye kitu kizuri japo...
ulikuwa hauna hela, lakini muziki wa sasa hivi ni muziki wa ujanja ujanja mwingi, ukiwa na akili nyingi, ukiwa mjanja basi unamake mkwanja.

Kwa hiyo naweza nikasema muziki wa sasa hivi una hela sana kuliko wa zamani lakini ili uzipate unatakiwa kuwa mjanja, unaweza ukawa unachana sana, unaandika sana lakini ukatoka bila,” alisema Nay.

Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi ukidumu kwa muda mrefu ni miezi mitatu, lakini nyimbo nyingi za zamani zitaendelea kuwepo kwa sababu wasanii wake walikuwa hawana ujanja ujanja, wanaandika kweli na wanazingatia kila kitu katika uandishi,” alisema Nay.

0 comments:

Post a Comment