Pages

Subscribe:

Tuesday, April 26, 2016

KALA JEREMIAH APATA MTOTO WA KIUME AMWITA...

Kala

Mpenzi wa msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amejifungua mtoto wa kiume Jumamosi hii, nakupewa jina, ‘Alama’
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu ya jana, Kala amesema jina Alama limetokana na jina lake la zamani, ‘Mark’. “Kusema kweli nafuraha sana kupata mtoto wa kwanza wakiume,” alisema Kala. “Mama yake nipo naye sema...
sikainaye ila ni mtu wangu wa muhimu sana kwa sababu ameniletea kiumbe,”
 
Aliongeza, “Mwanangu anaitwa Alama, vyovyote unavyotaka kumuita, ukitaka umwite alama ya kuuliza, sijui nini wewe tu. Nimempa jina hilo kwa sababu ni jina langu ambalo nilikuwa nalitumia wakati nauza mtumba, hata marafiki zangu wanajua nilikuwa naitwa Mark, sema nikalibadili na kuliweka Alama, kwa kiswahili,”

0 comments:

Post a Comment