Joka
kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani limekutwa likiwa limekufa.
Chatu huyo alipatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia karibu na mti mkubwa uliokatwa katika kisiwa cha Penang. Linakisiwa kuwa na urefu wa takriban na mita 8 hivi sawa na futi 26 lilipatikana...
siku ya Alhamisi iliyopita. Kwa bahati mbaya joka hilo lilikufa Jumapili lilipokuwa likizaa, afisa anayesimamia ujenzi katika kisiwa hicho cha Penang, Herme Herisyam aliiambia BBC.
Kulingana
na daftari za kumbukumbu za Guinness, joka anayeshikilia rekodi ya dunia
anaurefu wa mita 7.67. Chatu huyo anayeitwa Medusa ana uzani wa kilo 158 na
anaishi katika jumba moja mjini Kansas City, Missouri Marekani.
Hata
hivyo joka huyo wa Malaysia ambaye alikuwa mkubwa zaidi yake hakuwa amepimwa na
kuthibitishwa kuwa mrefu zaidi kabla ya kufa kwake.
Herisyan
anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata
hivyo katika harakati za kumuokoa kutoka maficho yake inakisiwa kuwa aliumia na
hivyo akafa kabla hajafikishwa kwenye hifadhi ya wanyama alikotarajiwa kutuzwa
hadi ajifungue.
0 comments:
Post a Comment