Pages

Subscribe:

Monday, April 11, 2016

MIMI NA WEMA HATUJAACHANA ILA HATUA MAELEWANO MAZURI

Idris Sultan amezungumzia suala la video iliyosambaa ikimuonesha mpenzi wake, Wema akimbusu mwanaume mwingine.
“Ingetokea kwamba tupo kwenye party na kuna huyu jamaa ‘gay’ najua wakati mwingine ni kitu cha mchezo kumbusu mwanaume ‘gay’ haijalishi, wao ni nyoka wasio na sumu lakini inapotokea...
unapuuzia tu,” Idris alizungumka kwenye mahojiano na kipindi cha The Trend cha NTV ya Kenya.

“Lakini pale video inapowekwa mtandaoni na kila mtu anaiongelea na kila mtu anakuja kwangu kusema ‘mwanamke wako anachukuliwa tu na huwezi kufanya chochote, sasa wanaanza kuniita bwege na vitu kama hivyo, huwezi hata kumtawala mwanamke wako, huwezi hata kumkataza kufanya hili na lile na ninapoongea naye hanijibu vizuri,” alisisiza.

“Niliongea naye na akaniletea kiburi, alipokuwa hivyo nikasema nilitarajia walau ungeelewa, sijisikii vizuri kuhusu hili. Ninajisikia vibaya si kuhusu busu lenyewe ni kuhusu kwanini ipo mtandaoni, ni chuki kiasi gani ninazopata kutokana na hili, hakuwa anapata chuki kama niliyokuwa napata kwasababu ya video hiyo.

Baada ya kusema nimechoka na kutoheshimiwa, watu ndio wakaelewa kuwa Idris anakuwa mwanaume wakati mwanzoni walisema ‘anakuwa kama mwanamke sasa’ kwasababu nini mwanamke wake anachofanya,” aliongeza Idris.
Idris alipoulizwa kama ameachana na mrembo huyo Idris alisema hawana maelewano mazuri tu.

0 comments:

Post a Comment