Pages

Subscribe:

Thursday, September 24, 2015

BARAKAH DA PRINCE APATA USIMAMIZI MPYA WA KAZI ZAKE

Star wa muziki Barakah da Prince amelitolea ufafanuzi suala la yeye kuingia katika makubaliano ya usimamizi wa kazi zake za muziki na kampuni nyingine ambayo imeonekana kumvutia star huyo nchini.  Pamoja na kusitisha huko bado imeonekana kuwa hakuna utaratibu rasmi uliofanyika kusitisha...
makubaliano na Kid Bway, meneja aliyekuwa akifanya naye kazi tangu kuanza safari yake kimuziki.

Barakah ameeleza kuwa, chanzo cha taarifa hizo ambacho ni picha zilizoonekana akisaini mkataba, hazihusiani na mambo ya kubadilisha usimamizi, akiambatanisha pia na kauli tata kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo binafsi atakaa chini na Kidbway kuweka sawa hivi karibuni.

Kwa upande wa Kid Bway kuhusu sakata hilo, binafsi amesema hafahamu lolote juu ya msanii wake kusaini mkataba mpya, akiwa ameziona picha katika mtandao kama watu wengine tu.

0 comments:

Post a Comment