Pages

Subscribe:

Thursday, September 10, 2015

WANATAKA KUUFUNGIA WIMBO WANGU KISA NIMEONGEA UKWELI... ASEMA ROMA

roma new pic
Saa chache baada ya wimbo mpya wa Roma ‘Viva Roma viva’ kutoka September 9, rapper huyo amedai kuwa ametishiwa wimbo huo kufungiwa.
Kupitia Instagram, majira ya saa mbili usiku Roma aliandika;
“WANATAKA KUIFUNGIA NYIMBO YANGU!! KISA TU NIMEONGEA UKWELI!! INANIUMA SANA NATAMANI... HATA KULIA NIKIONA UKWELI HAUPEWI NAFASI!! NIOMBEENI NA MNIKUMBUKE KWENYE SALA ZENU NDUGU ZANGU!! Viva Roma viva”
ro
Bado haijafahamika sababu ya wimbo huo kutaka kufungiwa, na Roma hakupatikana kwenye simu yake nilipomtafuta kwaajili ya kuzungumza nae kuhusu swala hilo.

0 comments:

Post a Comment