Pages

Subscribe:

Thursday, September 17, 2015

SAUTI SOL WAANZA KUMWINDA JOHN LEGEND


Kundi la muziki la Sauti Sol limeanzisha kampeni maalum yenye lengo la kumvuta staa wa kimataifa John Legend kutoka Marekani, lengo likiwa ni kukamilisha mpango wa kufanya naye remix ya ngoma yao ya 'Isabella'.
Sauti Sol wameamua kuendesha kampeni hiyo kwa njia ya mitandao ya kijami, wakitumia kwa sehemu kubwa jukwaa la mtandao wa Instagram kuchochea kampeni hiyo kwa kutumia hashtag ya #JohnLegendForIsabellaRemix ambayo itaendeshwa kwa siku 30, kabla ya kufanya...
mawasiliano rasmi na msanii huyo.
Kutokana na nguvu kubwa ya mitandao kama hiyo katika kuunganisha watu, na kutokana na ubora na uzuri wa rekodi kama Isabella, mastaa hao wanaamini kuwa mpango huo utawaleta karibu na kuweza kufanikisha mpango huo.

0 comments:

Post a Comment