Pages

Subscribe:

Saturday, September 19, 2015

DAVIDO ATHIBITISHA UJIO AWA COLLABLE YAKE MPYA NA JOH MAKINI

Davido amethibitisha kumshirikia rapper wa Tanzania kutoka kundi la Weusi, Joh Makini kwenye track yake mpya ambayo bado hajataja jina. kwenye tweet yake siku ya jana Davido aliandika...


DAVIDO X JOH MAKINI COMING SOON

Hii inakua collabo ya tatu ya Davido na wasanii wa Tanzania, Alithibitisha ujio wa collabo alioshirikishwa na Alikiba na kuweka wazi kuwa ilikua inakuja collabo nyingine na Diamond Platnumz wakati wa Tuzo za MAMA.

Kwa upande wa Joh Makini, Mwaka 2015 unazidi kuwa mwaka mzuri zaidi hasa baada ya video yake “Nusu Nusu” kupokelewa vizuri na kupata airtime kwenye vituo vikubwa kama ‘MTV Base’ pia kupata Collabo na wasanii wakubwa Afrika, hadi sasa tayari amekamilisha collabo na Video yake na rapper wa Afrika kusini AKA, na sasa anafanya collabo nyingine na rapper K.O ambaye anatoka Afrika kusini pia.

0 comments:

Post a Comment