Pages

Subscribe:

Monday, April 4, 2016

JINSI ZIDANE ALIVYO WEZA KUSHINDA EL CLASSICO YAKE YA KWANZA


Ilikuwa ni Clasico ya namna tofauti na historia. Barcelona walishindwa kuimudu timu ya Real Madrid ambayo ipo kwenye njia panda ya maendeleo chini ya Zidane.
Barca Blaugrana walishindwa kucheza kwa mfumo wao na ufundi uliojengwa na Luis Enrique, walishindwa kuwasha moto wao wa siku zote. Madrid walikamilisha kazi, lakini haikuwa kazi rahisi.

Sergio Ramos alionywa mara kadhaa kabla ya kuoneshwa kadi nyekundu. Lakini nyota wa Barca hawakukata tamaa, walipambana kusaka bao hadi walipopata goli la kwanza kupitia Gerard Pique. Barca waliendeleza falsafa yao ingawa walizidiwa kwa...
namna fulani - Johan Cruyff - ambaye alikumbukwa muda wote wa mechi - asingefurahishwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar kushindwa kufunga.


Suarez hakuwa katika ubora wake wa siku zote; Neymar hakuweza kupiga hata shuti moja golini; Messi pamoja na uwezo wake mkubwa hakuweza kuzifumania nyavu - hivyo Barca wakapata goli kupitia Gerard Pique.

Haikuwa Clasico ya wacheza fulani nyota kama ilivyo siku zote, timu zote zilicheza kwa kujituma, baada ya Karim Benzema kutupia, hadi mabeki wa Real Madrid walionyesha kuamka zaidi.


Jambo mojawapo ambalo lingeweza kuamsha tabasamu la Cruyff ni kuingia kwa Arda Turan kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic kipindi cha pili. Luis Enrique alionesha ujasiri kumuingiza Mturuki huyo kufanya jukumu muhimu dimbani. Hawezi kucheza katika kiwango kikubwa kama cha Rakitic lakini ni mtu asiyetabirika.

Lakini kwa bahati mbaya, mabadiliko hayo hayakuzaa matunda yaliyotarajiwa. Uamuzi wake hakulipa hata baada ya kutolewa kwa Sergio Ramos dakika saba zikiwa zimesalia. Kwa mara ya kwanza Madrid na si Barca walikuwa na ari njema.
Dakika za majeruhi mashabiki wa Los Blancos walinyanyuka vitini kushangilia bao safi kabisa la ushindi kutoka kwa Cristiano Ronaldo, aliyefunga kwa pasi nzuri kutoka kwa Gareth Bale, Lo! zawadi iliyoje kutoka kwa nyota huyo raia wa Wales?

Zinedine Zidane ameonyesha ufundi wake kwa kushinda mechi yake ya kwanza El Clasico, Ni dhahiri kikosi cha Real Madrid kimeonyesha mabadiliko ya hali ya juu sana.

0 comments:

Post a Comment