Pages

Subscribe:

Monday, June 27, 2016

HADITHI: NYUMA YA MACHOZI (sehemu ya tisa) 09


MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
ILIPOISHIA:
“Jimmy ukiifanya kazi kwa ufanisi nitakupa laki mbili.” “Utani huo sister!”
“Sina utani kwa jambo nitakalo kuahidi.”
“Sawa, wacha nikuache uendelee na mambo mengine.”
Jimmy aliondoka na kumuacha Kilole akitengeneza nyumba kwa ajili ya sherehe ya kutengeneza ya birhtday yake. Sebule aliipamba na kupambika ikawa katika muonekana wa kupendeza.
SASA ENDELEA...
*******
Majira ya saa mbili usiku kila kitu kilikuwa kimepangwa sehemu yake, Kinape na mpenzi wake nao walikuwepo kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Kilole.
Ilikuwa sherehe iliyozuka kama uyoga, ule ulikuwa mpango...
wake maalumu wa kuhakikisha nasambalatisha penzi la Kinape na Happy pia kumrudisha mikononi mwake. Kabla ya sherehe kuanza simu ya Happy mchumba wa Kinape iliita, aliipokea na kuzunguza. 

“Haloo.. eeh .. Nipo kwa Kinape... Kuna sherehe ya kuzaliwa shemeji yake...Eeeh!... Nini? Acha utani.. Mungu wangu nakuja...Aah.. lazima nije?”
“Vipi?” Kinape na Kilole waliuliza kwa pamoja baada ya kumuona Happy akitokwa na machozi huku ameshikilia mikono kichwani. “Mama,” alijibu kwa mkato.
“Mama kafanya nini?”
“Kavamiwa na majambazi walitaka kumpora gari.”
“Wamemjeruhi?”
“Wanasema hawajamjeruhi, wanaomba niendelee na sherehe lakini lazima nikamuone mama kisha nitarudi.” 

“Kinape mpeleke mwenzako,” Kilole alijifanya mwema.
“Hapana dada ninyi endeleeni tu, nitarudi muda si mrefu, inaonekana tatizo siyo kubwa, nitakwenda peke yangu.” Happy aliwatoa wasi.
“Hapana mpenzi lazima nikupeleke,” Kinape alisema.
“Lakini kama umesema mama hana tatizo basi wacha nianze sherehe na Kinape ukirudi tutaungana pamoja,” Kilole alitumia nafasi ile kumbakiza Kinape.
“Kweli kabisa dada, nisiharibu utaratibu wa sherehe kwa vile ilikuwa ndiyo inaanza.” “Ila shampeni utaifungua ukirudi.”
“Hakuna tatizo.”

Kinape alimsindikiza Happy mpaka nje, baada ya kuingia kwenye gari na kuondoka alirudi ndani kuendelea na sherehe ya mtego aliyoandaliwa yeye bila kujijua. Wakati Kinape akitoka nje kumsindikiza mpenzi wake, Kilole alitumia nafasi ile kumuwekea dawa ya kulevya kwenye juisi.

Kinape aliporudi alikaa kwenye kochi na kuchukua glasi ya juisi na kunywa kidogo huku akimtupia swali Kilole kuvuta muda labda Happy atawahi kurudi. Kilole alifurahia moyoni na kuona mpango wake umekuwa rahisi tofauti na alivyopanga wa kumtumia Jimmy kumtoa Happy kwa simu ya uongo ili kitendo kifanyike kwa haraka. Lakini simu kutoka kwao kidogo imfanye apige yowe la furaha.
“Shemu, Deus anajua kama leo ni tarehe yako ya kuzaliwa?”
“Anajua na muda si mrefu nitakufanyieni bonge la surprise na mchumba wako.” “La nini tena, mbona umenirusha roho.”
“Utaliona muda si mrefu.” “Nigusie kidogo.”
“Ukijua haitakushtua, nataka uamini nakupenda shemeji yangu.”
“Mmh! Haya.”

Kinape alisema huku akichukua glasi ya juisi na kupiga funda zingine tatu na kurudisha glasi chini. Mara alianza kuhisi kichwa kizito, alijitahidi kushindana na hali iliyomtokea kila macho yalizidi kufumba. Kilole alifurahi kuona kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.

Taratibu Kinape alijilaza kwenye kochi, kwa hatua ile Kilole aliona tayari mpango wa awali umekamilika. Alikumbuka mlango upo wazi alikwenda kuufunga, kisha alimpigia simu Jimmy.
“Haloo Jimmy.”
“Vipi Sister, nipige ile simu?” “Hapana, njoo nyumbani haraka.”
“Nipe dakika sifuri.” 

Alipokata simu mlango uligongwa, alijua Jimmy amefika, alitoka hadi mlangoni na kufungua. Alishtuka kumuona Happy mbele yake, alipotaka kuingia ndani alimshika kifuani na kumrudisha nyuma.
“Vipi dada!” Happy aliuliza kwa mshangao.
“Kinape kakufuata.”
“Kanifuata vipi wakati nimemwambia narudi?” “Amesema huenda mama yako kapata matatizo makubwa.” “Jamani! Sasa kapitia wapi mbona sikumuona?”
“Kwa kweli sijui kitu, nimembembeleza akusubiri kakataa.”

“Kwa nini asinipigie simu?”
“Mmh! Siwezi kujua.” Happy aliamua kumpigia simu Kinape mbele yake, baada ya muda simu iliita ndani.
“Mbona simu yake inaita ndani?”
“Aliisahau kutokana na papara zake.”
“Sasa nikimfuata si nitapotezana naye, bora nimsubiri ndani.” “Happy, kutokana na king’ang’anizi cha mpenzi wako nimeamua kuahisha sherehe mpaka jumamosi.”
“Hata hivyo siwezi kusumbuka kumfuata, wacha tu nimsubiri,” Happy alisema huku akitaka kuingia ndani.

 “Happy kuwa muelewa, Kinape baada ya kuondoka nimemweleza nimeamua kuahirisha sherehe na yeye alisema hatarudi mpaka kesho. Sasa ukimsubiri itakuwaje?” “Mmh! Wacha nimuwahi,” Happy alisema huku akigeuka na kuondoka. Kilole hakuingia ndani mpaka aliposikia sauti ya gari la Happy likiondoka, wakati huo Jimmy alikuwa amefika.
“Ooh! Jimmy karibu ndani.”

“Asante,” Jimmy alijibu huku akiingia ndani. Alipofika sebuleni alishangaa kukuta kuna kitu kama sherehe, mbele kulikuwa na keki kubwa iliyoandikwa Happy Birthday Kilole na pembeni yake kulikuwa na chupa kubwa ya shampeni. Sehemu nyingine kulikiwa na vinywaji ndani ya glasi. Alipoangalia kwenye kochi alimuona Kinape ameutwanga usingizi.

“Vipi Sister naona ulikuwa na sherehe ya kuzaliwa kwako?”
“Ndiyo, lakini sicho nilichokuitia.”
Jibu lilimfanya Jimmy asiulize kitu zaidi ya kusubiri alichoitiwa.
“Ndiyo sister lete maneno?”
“Kazi niliyokuitia sasa imekamilika nataka ufuate maagizo yangu, malipo yako nilikuambia kiasi gani?”
“Laki mbili.”

“Nitakuongezea hamsini, itakuwa laki mbili na nusu.”
“Hakuna tatizo,” Jimmy alikubali bila kujua ni kazi gani. Baada ya kuhakikisha mlango ameufunga vizuri alimuomba Jimmy amsaidie kumuingiza ndani Kinape.
Walisaidizana kumwingiza chumbani, Kilole alimpeleka katika chumba chao cha kulala kisha walimlaza kitandani. Baada ya kumlaza walitoka mpaka sebuleni kupanga mipango yao. “Sasa sikiliza kazi niliyokuitia ni hii.”
“Kazi gani?”

“Nataka unipige picha kwenye tukio lote nitakalokuwa nalifanya kisha utaenda kunisafishia na kuniletea picha zote, sawa?” “Picha za tukio gani?”
“Nitakalo lifanya muda mfupi usilishangae nina sababu zangu ila nakuomba unifichie siri hii.”
“Hakuna tatizo.” 

“Basi subiri.” Kilole alisema huku alielekea chumbani kwake, Jimmy alibaki akijiuliza anataka kupewa kazi gani. Baada ya muda Kilole alirudi akiwa katika vazi la kanga moja iliyoonesha hakuwa na nguo nyingine ndani. “Jimmy,” alimwita kwa sauti ya chini. “Na..na..aam,” Jimmy alionekana kuchanganyikiwa na umbile la Kilole lililokuwa la utata kwa mwanaume shababi.
“Jimiiii, utaiweza kazi kweli?”
“Kwa nini?”
“Umeona negative umechanganyikiwa ukiona picha si utashindwa hata kuifanya hiyo kazi.”
“Niwaweza tu wala usihofu.” “Umeisha andaa kamera yako?”
“Ndiyo.”
“Basi njoo chumbani.”

Jimmy kabla ya kwenda chumbani alifikiria ameitwa na Kilole kufanya naye mapenzi kwa kisingizio cha kupiga picha. Japo alijua mke wa mtu sumu lakini kwa mwanamke aliyeumbwa akaumbika kama Kilole ilikuwa sawa na nzi kufia juu ya kidonda. Uchu wa ngono ulimjaa na kujiona kama mbwa anayejipeleka mwenyewe kwa chatu, alitembea huku mwili wake ukiongezeka joto la matanio. Alipoingia chumbani alishangaa kumuona Kinape amelala kitandani hajitambui akiwa mtupu. Hali ile ilimshtua na kujiuliza kulikoni kuwa vile. Kilole alikwisha msoma Jimmy, ilikumtoa hofu alimwambia: 

“Jimmy utakachokiona humu ndani kiache kama ulivyokiona, nikisikia chochote tutaonana wabaya, Kabla ya mimi kulikimbia jiji nitaanza na wewe.
” Kilole alitoa onyo kali kwa Jimmy. “Siwezi kufanya hivyo.”
“Sawa, sasa naomba upige picha kila tendo nitalofanya na Kinape.”
“Tendo gani?”

“Usiulize andaa kamera yako,” Kilole alikuwa mkali kidogo. Jimmy hakuongeza swali zaidi ya kufuata maelekezo, muda wote bado alikuwa gizani kutokana na hali iliyokuwemo mule chumbani kwa Kinape kulazwa chali kitandani akiwa mtupu na sehemu zake za siri zilikuwa zimenyanyuka. Kabla hajapata jibu Kilole aliitoa kanga iliyostiri mwili wake na yeye kubakia mtupu.
“Jimmy,” alimwita huku akipanda kitandani.
“Aah...Eeeh...Na..naa..m.”

“Naona umepagawa, sasa kila hatua piga picha, sawa?”
“Sawa,” Jimmy alijibu macho yamemtoka pima.
Jimmy alimshangaa Kilole mambo ya aibu aliyokuwa akiyafanya mbele yake bila haya, alifanya mapenzi na Kinape aliyekuwa hajitambui kwa kumkalia juu yake. Ajabu Jimmy alijisahau kazi aliyopewa ya kupiga picha na kujikuta akipandwa na mzuka wa ngono. Alimshangaa Kilole mke wa mtu kufanya mpenzi na shemeji yake ambaye alionekana amelewa kupita kiasi. 

Aliona heri kama amezidiwa angemweleza yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu asiyejitambua. Kilole alipofumbua macho alimshangaa Jimmy aliyekuwa amesahau kazi aliyomtuma. “Jimmiiiii,” sauti kali ya Kilole ilimshtua Jimmy aliyekuwa akiangalia Blue print live bila chenga.
“Jimmy, umeisha piga picha?”
“Samahani Sister,” Jimmy alibabaika.
“Samahani nini Jimmy, kazi imekushinda?”
“Ha..ha..pana,” Jimmy alibabaika hata kamera alikuwa ameweka chini ili afaidi vizuri mambo ya wakubwa. Aliiokota na kujiandaa kupiga picha huku akitetemeka.
”Naomba upige picha kila hatua sawa?”
“Sawa.” Kilole alianza zoezi upya la kijidhalilisha mbele ya Jimmy, naye alipiga picha kila hatua.

Baada ya zoezi lake kukamilika, alimuomba Jimmy amuoneshe picha zote. Alichagua zinazofaa na zingine kuzifuta kisha alimuomba Jimmy atoke akamsubiri sebuleni. Jimmy alitoka akiwa katika hali mbaya baada ya kuzidiwa na ashki, kuna kipindi aliwaza hata ambake Kilole. 

Lakini alikumbuka alikuwa kazini na kazi ile ya hatari aliahidiwa pesa nyingi, alikaa sebuleni kumsubiri Kilole ambaye alikuja baada ya robo saa akionesha ametoka kuoga na kuvalia nguo ya kulalia.

“Jimmy, mzigo wako huu hapa, hizi ni laki na nusu, hamsini za kusafishia na laki moja adivansi ukileta picha zangu nakumalizia laki na nusu. Ila kuna zawadi yako kubwa kama utakuwa msiri, kuna kazi nyingine ya milioni moja.”
“Wacha!” “Wewe tu kuonesha uaminifu.” 

“Basi dada kesho saa nne nakuletea mzigo wako, andaa fedha yangu tu.”
“Hakuna tatizo, tutaonana kesho, lakini chonde chonde siri hii asijue mtu yeyote.”
“Nakuhakikishia siri hii itabakia kwa watu wawili mimi na wewe tu.”
“Haya, usiku mwema.”
Itaendelea...

0 comments:

Post a Comment