Pages

Subscribe:

Wednesday, June 29, 2016

FID Q AUELEZEA USHINDI WA BLACK COFFEE ASEMA KUNA HIT "SONGS" NA BEST "SONGS"


13408916_563958783784867_421936358_n
Fid Q amesema kilichowafanya watu washangae ushindi wa Black Coffee kwenye tuzo za BET mwaka huu na kuwashinda waliokuwa wakitarajiwa zaidi kushinda kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, ambao ni Wizkid, Diamond au AKA, ni kutokujua kuwa kuna tofauti kubwa kati ya ‘hit songs na best songs.’

“Hizi awards nyingi zinachaguaga best song sio hit song, nikimaanisha ya kwamba Prakatatumba ile ni hit song lakini sio...
best African song,” Fid alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka.

“Sasa wenyewe walishazoea kwamba msanii awe tu anahit asiwe best. Mfano watu kama akina Black Coffee ndio tunaweza tukawa hatuwatambui huku lakini kazi zake zinafika mbali zaidi kuliko ambazo sisi tunazitambua. Kwasababu watanzania tunamtambua Yemi Alade, Wizkid, Diamond, AKA tumemaliza lakini tulikuwa hatujamzingatia Black Coffee kwasababu anafanya aina fulani ya muziki ambayo sisi watanzania hatuusikilizi sana,” alisisitiza.

Amesema nyimbo za DJ huyo zinachezwa mno kwenye club za Afrika Kusini na nchi zingine.
Kwa upande mwingine Fid amemmwagia sifa Diamond kuwa ni msanii anayejituma na hivyo alistahili kabisa kushinda tuzo hiyo.

“Anawekeza sana kwenye sanaa yake, anatumia muda wake mwingi sana katika kuhakikisha kuwa anajiendeleza vyema. Kwahiyo kwa juhudi kama zile nahisi kwa namna moja ama nyingine walipaswa kumtazama pia lakini haikuwa bahati yake.”

0 comments:

Post a Comment