Pages

Subscribe:

Monday, June 27, 2016

NAY WA MITEGO KUWATAMBULISHA ANAO WASIMAMIA

Msanii wa Hip Hop, Nay wa Mitego amepanga kuwatambulisha rasmi wasanii ambao anawasimamia chini ya label yake ya ‘Free Nation 966′. Nay wa Mitego ambaye amedai kuwa yeye ndio msanii wa kwanza kabisa kuanza kuwasimamia wasanii wengine alifunguka hivi karibuni kuwa...
umefika muda muafaka kuwatambulisha wasanii hao rasmi
nay
“Unajua mimi ni msanii wa kwanza kuanza kusimamia wasanii wenzangu, mpaka sasa nina wasanii watatu ambao wapo chini ya Free Nation, lakini kwa kuanza tutaanza na mmoja ambaye tushakamilisha naye kila kitu anaitwa Tiki, nadhani Label yangu itakuwa na utofauti na Label nyingi sababu moja mimi ni mfanyabiashara hivyo hata msanii naye mleta lazima anaiingizie pesa huku akiwakonga mashabiki zake kwa muziki mzuri” Nay alielezea.

Diamond pia hivi karibuni aliwatambulisha rasmi Harmonize, Raymond, Rich Mavoko na Queen Darleen chini ya label yake ya WCB, Ommy Dimpoz pia alimtambulisha Nedy Music chini ya label yake ya PKP na Shilole pia amemtambulisha msanii mpya Gaucho chini ya label yake ya ‘Shilole Entertainment’.

0 comments:

Post a Comment