Pages

Subscribe:

Monday, June 27, 2016

BAADA YA KUKOSA PENATI MESSI ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Baada ya Chile kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa alfajiri ya ya kuamkia Jumatatu ya  June 27 kwa  kuifunga Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penati huku nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa Argentina Lionel Messi akikosa  penati ikiwa ni mara ya pili ndani ya miaka miwili mfululizo.

Argentna ikipoteza mchezo wa fainali ya Copa America mbele ya Chile ‘La Roja’,hatimae mshambualiaji huyo wa Barcelona ameamua kuachana na timu yake ya taifa kwa kutangaza...
rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina.

Baada ya game dhidi ya Chile, nyota huyo mwenye miaka 29 amekiambia kituo cha TYC Sports kwamba, amaisha yake ya soka la kimataifa yamefika mwisho.
“Kwasasa timu ya taifa basi tena. Baada ya kupoteza fainali nne sitaendelea tena kuitumikia timu ya taifa. Naamini tayari maamuzi yameshafanyika. Nimechukua muamuzi huu kwa ajili yangu pamoja na watu wengu waliotaka iwe hivi. 

Nimepambana sana, lakini ninaondoka nikiwa sijafanikiwa”.Alisema Messi mwenye umri wa miaka 29.
Video-Messi akitangaza uamuzi wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina.

Je Messi atabadili maamuzi yake? Au ndiyo basi tena na amemaliza maisha yake ya soka bila kushinda kombe la dunia,tusubiri tuone

0 comments:

Post a Comment