Pages

Subscribe:

Thursday, June 30, 2016

DARMIAN SOUL ASIMULIA ALIVYOPATA TABU NA NGOMA YAKE KAUMBA

4K0A8812
Damian Soul amesema wimbo wake ‘Kaumba’ aliomshirikisha Vanessa Mdee ulimtoa jasho haswaa – kama sio kamasi kabisa. Amedai kuwa wimbo huo ulizaliwa alipokuwa nchini Kenya mwaka jana kwenye kipindi cha Maisha Superstars. Anasema alitaka kufanya wimbo na Nameless aliyemwambia kuwa...
anaupenda sana wimbo wake ‘Dua la Kuku’ kiasi cha kumshawishi waufanyie kitu lakini alishauri wafanye kitu tofauti.

Anasema ndipo walipoenda kwa producer Sappy na kuanza kukuna kichwa kutengeneza wimbo wao hadi pale walipopata idea ya Kaumba na wakawa na beat chorus. Aliporudi Dar alianza kuufanyia kazi wimbo huo ikiwemo kuandika mashairi na katika moja ya mazungumzo na Joh Makini alisaidiwa kupata mistari ya kwanza iliyomshawishi kumalizia kuandika.
Alimtumia wimbo huo Vanessa kumuomba amshirikishe na Vee anadai aliupenda tu alipousikia mara ya kwanza.

“Nilikuwa nausikiliza nikiwa naenda Nigeria nikaweka hiyo song on replay nikalala hivi, I am telling you nilikuwa nashindwa kulala,” anasema Vanessa.
Hicho kilimpa moyo Damian na kudai kuwa hakuna kitu kizuri kama mtu unayetaka kumshirikisha akiupenda wimbo na sio kukubali kufanya kwasababu ya heshima.

0 comments:

Post a Comment