Pages

Subscribe:

Sunday, June 19, 2016

HEMED PHD AELEZA MADHARA YA KUTOKA NA MASTAA


Hemed PHD3
Muuza sura kwenye filamu za Kibongo, Hemed Suleiman ‘Hemed PHD’ amefunguka kuwa japo ni staa na mtu maarufu Tanzania lakini hata siku moja hajawahi kufikiri kuwa atakuja kujihusisha kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa kike kutoka Bongo kwa sababu anafahamu madhara yake.

Akizungumza, PHD aliongeza kuwa madhara ya kutoka na staa kimapenzi husababisha vyombo vya habari kuwamulika wahusika muda wote jambo ambalo yeye halipendi ukizingatia anafuata misingi ya...
dini yake ya Kiislamu inayomfanya aamini kuwa uhusiano ni suala binafsi ambalo halihitaji kushereheswa na watu.

“Unajua vyombo vya habari vinapofahamu kuwa unatoka na staa fulani vinaanza kukuandama wewe pamoja na huyo mpenzi wako. Si kitu kizuri kwa sababu mnapotofautiana pia vinaanza kuwazungumzia jambo ambalo wakati mwingine linaweza kusababisha hata msirudiane kutokana na misteki tu ndogo. So mimi sipendi kabisa maisha yangu yamulikwe ndiyo maana nimejiweka kando kwenye suala zima la uhusiano kutoka na staa,” alisema PHD.

0 comments:

Post a Comment