Pages

Subscribe:

Wednesday, June 29, 2016

SAUTI SOL: MAMBO YA DIAMOND NA ALIKIBA NI SIASA YA TANZANIA HATUONI SHIDA KUFANYA NAO KAZI WOTE

Member wa kundi la Sauti Sol, Savara amesema kufanya kazi na Alikiba haimaanishi kuwa wanamkubali zaidi kuliko Diamond. Kundi hilo lilifanya wimbo Unconditionally Bae na Alikiba uliofanya vizuri. “Mambo ya Alikiba na Diamond hiyo ni siasa ya Tanzania,” Alidai member wa kundi hilo.

Savara amekiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka aliyeuliza iwapo kundi hilo linaona kuwa uimbaji wa Alikiba unaendana zaidi na mtindo wao kuliko wa Diamond.“Mimi ni msanii, yule ambaye... anakuja wa kwanza na yule ninayefeel vibe yake nitafanya naye muziki, muziki utafanywa kila siku, haijalishwi unafanya na nani, mimi nitafanya hata collabo na Diamond, tutafanya collabo na msanii mwingine yeyote,” amesema.

Pia Savara amesema watafanya wimbo na Vanessa Mdee huku wakipenda pia kumtumia Nahreel siku za usoni kushiriki kutengeneza nyimbo zao. Lakini pia amedai kuwa ametengeneza wimbo wa Joh Makini.

0 comments:

Post a Comment