Pages

Subscribe:

Tuesday, June 21, 2016

POST YA DIAMOND YAWATOA UDENDA MASHABIKI


diamond342
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametupia picha hiyo hapo juu kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na kundi la P Square pamoja na uongozi wake,  wakiangalia kazi hiyo kama kufanya mapitio na kuandika kuwa anasikia harufu ya hit song. Diamond Platnumz ingawa hajaweka wazi lini kazi hiyo inatoka lakini kuna kila dalili kuwa kazi hiyo inaweza kutoka...
wiki hii kwani tayari ameshaanza kuwaweka sawa mashabiki wake kukaa tayari na kuwa karibu na mitandao yake kwa ajili ya kazi hiyo.

Kitendo cha Diamond kupost picha hiyo na kuandika maneno hayo kumeibua hisia mbalimbali zenye furaha kwa mashabiki wake ambo wengi wameonyesha kuwa na furaha na wakitabiri kuwa huenda ikawa kazi kubwa kutokana na jinsi wanavyomuamini msanii wao na kusema kuwa hajawahi kuwaangusha.

0 comments:

Post a Comment